Wanasoka mashuhuri wamechuana kupinga njaa Pakistan na Haiti

Wanasoka mashuhuri wamechuana kupinga njaa Pakistan na Haiti

Umoja wa Mataifa umetumia mchezo wa soka ili kuwafikia wahanga wa majanga ya kimaumbile yaliyotokea katika nchi za Haiti na Pakistan ambako mamia ya watu waliathiriwqa vibaya.

Mchezo huo wa soka ambao umeratibiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP umeshuhudia wanamichezo nyota akiwemo Ronaldo na Zinédine Zidane wakishuka dimbani huko Athens wakiwa na ujumbe wa kutaka dunia kuongeza juhudi ili kufikia shabaya ya malengo ya maendeleo ya mellenia hasa lengo namba moja linalotaka kutokomeza njaa.

Mchezo huo ambao umeonyeshwa na vituo vya televisheni karibu nchi 30, umefanyika katika uwanja wa Karaiskakis chini ya wenyeji wa timu ya Olympics. Kwa upande wake Zidane amesema kuwa ulimwengu haupaswi kuwaacha wanachi wa Haiti na Pakistan wakiendelea kuteseka na hivyo lazima waungwe mkono kwa hali na mali.