CERF kupata dola milioni 358 kusaidia majanga

15 Disemba 2010

Mataifa 59 ambayo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa yamehaidi kutoa kiasi cha dola milioni 358 kwa ajili kutunisha mfuko wa dharura unaotumika kukabili majanga CERF.

Msaada huo umetangazwa wakati wa kongamano liliandaliwa kwa ajili ya kutunisha mfuko huo.

Kwa mara ya kwanza mashirika ya kirai na sekta binafsi zimehaidi pia kuupiga jeki mfuko huo.

Mkuu wa shughuli za misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos amesema kuwa kiasi hicho cha fedha ni mafanikio makubwa kwa mfuko huo hasa ikizingatiwa wakati huu wa hali ngumu ya kiuchumi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter