Skip to main content

Wakimbizi Nepal waendelea kupata makao mapya:UNHCR

Wakimbizi Nepal waendelea kupata makao mapya:UNHCR

Mpango wa kuwapa makao maelfu wakimbizi kutoka Nepal uliozinduliwa miaka mitatu iliyopita umeshuhudia kupatikana kwa makao kwa zaidi ya idadi wa wakimbizi iliyowekwa ya wakimbizi 40,000.

Hii ni baada ya mkimbizi kwa jina Devi Maya kuwa mkimbizi nambari 40,000 na kuwa miongoni mwa wakimbizi 198 waliosafirishwa kujiunga na familia zao nchini Marekani. Wakimbizi hawa wamekuwa wakiishi katika kambi ya Beldangi One nchini Nepal baada ya kukimbia ghasia.

Mwakilishi wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa nchini Nepal Stephane Jaquemet amesema kuwa mpango huu umepata mafanikio kufuatia kuungwa kwake mkono na serikali ya Nepal. Maelfu ya wakimbizi wameweza kupata makao kwenye nchi nane tangu mpango huu uzinduliwe mwaka 2007 huku zaidi ya wakimbizi elfu 34 wakipata makao nchini Marekani.