Skip to main content

Mwaka wa kimataifa wa watu wenye asili ya Kiafrika wazinduliwa

Mwaka wa kimataifa wa watu wenye asili ya Kiafrika wazinduliwa

Mwaka wa kimataifa wa watu wenye asili ya Kiafrika umezinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

Akiongea wakati wa kuzinduliwa kwa mwaka huu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa mwaka utachangia katika kumaliza ubaguzi dhidi ya watu wenye asili ya Kiafrika. Ban amesema kuwa mwaka huu wa kimataifa pia una lengo la kuleta haamasisho kuhusu heshima inayostahili kupewa mila na tamaduni za Kiafrika. Alisisitiza kuwa ni lazima ikumbukwe kuwa watu wa asili ya Kiafrika ni kati ya wale walioathirika na ubaguzi.Amesema kuwa mara nyingi waafrika wananyimwa haki za kimsingi kama vile afya na elimu na kuongeza kuwa uovu huo una historia mbaya na ndefu.