Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamaduni zinazowadhulumu wanawake zatajwa kuwa nyingi nchini Afghanistan

Tamaduni zinazowadhulumu wanawake zatajwa kuwa nyingi nchini Afghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaotoa huduma nchini Afghanistan UNAMA unasema kuwa tamaduni zinazodhuru ambazo zinaenda kinyume na haki za wanawake na wasichana bado ni nyingi nchini Afghanistan zikiendeshwa kwenye jamii zote kote nchini.

Kulingana na ripoti ya shirika hilo ni kuwa hatua za haraka zinaazowalinda wanawake na wasichana zinastahili kuchukuliwa hususan kubuniwa kwa sheria inayowalinda wanawake na wasichana kutoka na dhuluma. Kati ya tamaduni zinaoenda kinyume na haki za wanawake nchini Afganistan ni pamoja ndoa ya lazima , kutoa watoto wasichana kama njia ya kutatua mizozo , kutengwa kwa lazima na mauaji.