Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINURCAT yaondoka Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati lakini bado kuna changamoto: Ban

MINURCAT yaondoka Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati lakini bado kuna changamoto: Ban

Huku ujumbe wa Umoja wa Mataifa ukijiandaa kuondoka nchini Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati ifikapo mwishoni mwa mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki moon ameonya kuwa bado maeneo hayo yanakabiliwa na changamoto nyingi za binadamu.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)

Kwa kuomba kuwa uondolewe , Chad inasema kuwa inachukua jukumu la kuwalinda raia kupitia kwa kikosi ambacho kimepewa mafunzo na Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema kwamba bado hali katika eneo la kaskazini mashariki ya Jamhuri ya afrika ya kati inabaki kuwa mbaya huku Umoja wa Mataifa ukibaini kuwa kuna hatari katika masuala kadha yakiwemo ya kijamii , kiuchumi na kisiasa. Ameongeza kuwa MINURCAT ilikabaliwa na changamoto za ukosefu wa mawasiliano na hivyo haikuweza kuyatimiza vilivyo matakwa ya serikali. Lakini hata hivyo amesema ujumbe huo unaacha nyuma wataalamu waliopata mafunzo na ujunzi wao utakuwa wenye manufaa kwa nchi.