Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazidisha ushawishi wake kwa Ivory Coast ili kutanzua mzozo wa madaraka

UM wazidisha ushawishi wake kwa Ivory Coast ili kutanzua mzozo wa madaraka

Umoja wa Mataifa umeongeza ushawishi wake wa kidiplomasia kwa Ivory Coast ambayo inatia shaka huenda ikatumbukia tena kwenye machafuko makubwa kufuatia mzozo wa madaraka baina ya mahasimu wawili.

Licha ya miito kuendelea kupaza ikimtaka Rais Laurent Gbagbo ajiondoe madarakani, lakini hata hivyo ameendelea kusisitiza kuwa ndiye aliyeshinda kwenye uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita ambao tume ya taifa ya uchaguzi ilimtangaza mpinzani wake Alassane Ouattara kuwa ndiye mshindi.

Wakati baraza la Umoja wa Mataifa limekutana hii leo New York kujadilia hali hiyo, Mjini Abuja, Nigeria mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za frika magharibi Y. J. Choi amekuwa akitoa tathmini kwa viongozi wa ECOWAS waliokutana kwa dharura.

Bwana Choi amesema kuwa pamoja na kuongeza juhudi za kushawishi pande zote kujiepusha na jazba ili kuepusha hali yoyote ya vurugu lakini inatambua matokeo yaliyompa ushindi Ouattara. Pia Jumuiya Maendeleo ya Afrika Magharibi ECOWAS imetangaza kumtambua Alassane Ouattara kama Rais mteule wa Cote d´Ivoire, na kumtaka Rais Laurent Gbabgo kujiondoa madarakani.