Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakutana kujadili hali nchini Ivory Coast

UM wakutana kujadili hali nchini Ivory Coast

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo linakutana kujadili hali nchini Ivory Coast.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amelezea hisia zake na amekuwa akijadiliana na viongozi wa nchi za afrika kufuatia mzozo uliojiri baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa uars katika taifa hilo la afrika magharibi. Shughuli za mapatano zilizokuwa zikiongozwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki zimekamilika bila ya kupatikana kwa suluhu.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa kwa sasa taifa hilo linakabiliwa na uhaba wa bidhaa. Kwa sasa kila upande unaendelea kuchagua mawaziri huku UM ukiwasafirisha baadhi ya wafanyikazi wake kwenda nchini Gambia.