Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji kutoka Eritrea wazuiliwa nchini Misri :UNHCR

Wahamiaji kutoka Eritrea wazuiliwa nchini Misri :UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa karibu wakimbizi 250 raia wa Eritrea wanazuiliwa na waendesha bishara haramu ya binadamu katika eneo la Sinai nchini Misri.

Kwa sasa UNHCR inatoa wito kwa serikali ya Misri kuingilia kati na kusaidia kuachiliwa kwa wahamiaji hao ambao wamezuiliwa kwa karibu miezi miwili. Adrian Edwards ni msemaji wa Msemaji wa UNHCR :

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)