Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kanali wa DR Congo awekewa vikwazo na UM kwa mauaji

Kanali wa DR Congo awekewa vikwazo na UM kwa mauaji

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limemwekea vikwazo vya usafiri na vya kuzuiliwa kwa mali kanali mmoja wa kijeshi katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kutokana na mashataka ya kuhusika na mauaji aya watoto , kuwaingiza watoto jeshini pamoja na dhuluma za kimapenzi.

Mwakilishi maalaum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya watoto na mzozo Radhika Coomaraswamy amesema kuwa Kanali Innocent Zimurinda alihusika na mauaji ya halaiki na ubakaji wa wanawake na wasichana , akakataa kuwaachilia watoto kutoka jeshini na pia kuwanyima watu kupata mahitaji ya kibinadamu.

Mwakilishi huyo wa katibu mkuu anasema kuwa kila mwaka makundi yaliyojihami huwa yanawaiba watoto kutoka makwao na kuwabadili kuwa wanajeshi , wengine hushambulia mashule na kuwaua walimu , wengine huwadhulumu kimapenzi wasichana na wavulana na kuwaua watoto.

Wote hao wako kwenye orodha ya katibu mkuu na ni sharti wafanye uamuzi wa kushirikiana nao au wakabiliwe na vikwazo.