Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Alassane Outtara ashinda duru ya pili ya uchaguzi wa Rais Ivory Coast

Alassane Outtara ashinda duru ya pili ya uchaguzi wa Rais Ivory Coast

Mgombea wa Urais wa upinzani nchini Ivory Coast Alassane Ouattara ameshinda duru ya pili ya uchaguzi nchini humo kwa asilimia 54.1 dhidi ya mpinzani wake Rais wa sasa Laurent Gbagbo.

Ushindi huo umetangazwa leo na tume ya uchaguzi nchini humo . Rais Bagbo tayari ameshasema atapinga matokeo hayo kutokana madai ya udanganyifu na amekitaka chombo kikuu cha sheria nchini humo kubatilisha matokeo hayo.

Tume ya uchaguzi kwa mujibu wa sheria imekabidhi matokeo hayo ambayo kwa baraza la katiba ambalo limeyapokea na kuyathibitisha. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Youssouf Bakayoko ameyasema hayo baada ya kuyasoma matokeo hayo kwa waandishi wa habari kwenye hoteli yenye ulinzi mkali wa Umoja wa Mataifa UNOCI mjini Abidjan ambako mgombea Outtara ameweka makao.

Bagbo amepata asilimia 45.9 ya kura kwa mujibu wa matokeo yaliyosomwa. Uchaguzi huo una lengo la kuunganisha nchi hiyo mzalishaji mkubwa wa kakao baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoigawa mapande nchi hivyo mwaka 2002-2003.