Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya usalama nchini Ivory Coast bado ni tete:UM

Hali ya usalama nchini Ivory Coast bado ni tete:UM

Hali ya wasi wasi bado inatawala nchini Ivory Coast baada ya matokeo ya uchaguzi wa Urais kutotangazwa jana kama ilivyopangwa. Ripoti zinasema watu wane wafuasi wa kiongozi wa upinzani Alassane Ouattara wameuawa wakati wa shambulio la silaha kwenye moja ya ofisi zao zilizoko wilaya ya Yopougon mjini Abijan.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Jana jioni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alitoa taarifa maalumu na kusisitiza kwamba tume huru ya uchuguzi ya Ivory Coast ni lazima ikamilishe kazi yake na kutangaza matokeo ya awali bila kuchelewa zaidi.