ICC kuwasilisha mashitaka kwa Maafisa wa Serikali ya Kenya.
Mwendesha mashitaka Mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC amesema atawasilisha kesi mbili za machafuko ya baada ya uchaguzi nchini Kenya kwenye kitengo cha kesi cha mahakama hiyo katika muda wa wiki mbili.
Ocampo ambaye yuko Kenya kwa mkutano wa siku mbili wa mchakato wa maridhiano unaoongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema hataomba kibali cha kukamatwa kwa watu sita wanaoaminika kuhusika kwa kiasi kikubwa kwenye machafuko ya Kenya 2007. Amesema kesi hizo mbili zitakazowasilisha kabla ya Desemba 17 zitaelezea ushahidi wote uliokusanywa.
(SAUTI YA OCAMPO)
Hata hivyo mambo hayo bayana kabisa kwani majaji wanaweza kuidhinisha au kukataa ombi la Ocampo la kufungua mashitaka au hata kuligeuza kuwa kibali cha kukamatwa.Majaji watatathimini ushahidi wa Ocampo na kuamua endapo unatosha kuendelea na kesi , jambo ambalo litafanyika mwishoni mwa 2011 au mapema 2012, na kesi haitaweza kufanyika kabla ya mwishoni mwa 2012 au mapema 2013. Watu zaidi ya 1,300 waliowauwa katika machafuko na wengine laki sita kusambaratishwa na machafuko hayo.