Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ombi la msaada kwa ajili ya Somalia lazinduliwa Kenya:UNHCR

Ombi la msaada kwa ajili ya Somalia lazinduliwa Kenya:UNHCR

Mashirika ya misaada yanahitaji dola milioni 530 ili kukabiliana na matatizo ya kibinadamu yanayoendelea nchini Somalia.

Ombi la msaada huo limezinduliwa leo mjini Nairobi Kenya na kamishina mkuu wa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres na mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini Somalia Mark Bowden.

Ombi hilo kwa ajili ya mwaka 2011 linahitaji dola zaidi ya milioni 529 kwa ajili ya miradi 229, 15 ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na 90 ya mashirika ya kimataifa na yasiyo ya kiserikali ili kukabiliana na mahitaji ya dharura nchini Somalia. Jayson Nyakundi na taarifa kamili

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)