Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika siku ya ukimwi duniani pamoja na mafanikio, juhudi zaidi zinahitajika kupambana na ugonjwa huo:UM

Katika siku ya ukimwi duniani pamoja na mafanikio, juhudi zaidi zinahitajika kupambana na ugonjwa huo:UM

Umoja wa Mataifa unaungana na dunia nzima leo kuadhimisha siku ya kimataifa ya ukimwi, kauli mbiu ya mwaka huu ni fursa na haki za binadamu.

Kauli mbiu hii inaelezea kwamba kila mtu aliyeathirika na ukimwi ni lazima ahakikishiwe fursa ya kuzuia virusi vya HIV, huduma, tiba na msaada bila kubaguliwa au kuhukumiwa.

Katika kuunga mkono kaulimbiu hiyo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS, mfuko wa utafiti wa ukimwi AMFAR na kampeni za kupambana na ukimwi wamezindua kampeni iitwayo washa kwa ajili ya haki kwa lengo la kumulika haki muhimu ambazo wote tunahitaji na kuendelea kupigia chepuo haki za binadamu kwa walio na virusi vya HIV.

Akisisitiza kauli hiyo mkurugenzi mkuu wa wa WHO Margareth Chan amesema haki ya huduma za afya ni muhimu katika vita dhidi ya ukimwi.

(SAUTI YA MARGARETH CHAN)