Skip to main content

Mabadiliko ya sheria yatasaidia katika vita vya ukimwi:IPU

Mabadiliko ya sheria yatasaidia katika vita vya ukimwi:IPU

Rais wa muungano wa wabunge IPU ambaye pia ni spika wa bunge la Namibia Dr Theo-Ben Gurirab akizungumza leo katika siku ya kimataifa ya ukimwi amesema kwa zaidi ya miaka 20 siku ya ukimwi duniani inatukumbusha kuwa ugonjwa huo bado uko nasi nab ado kuna kibarua kigumu kuutokomeza.

Amesema mfano katika bara la Afrika ambako ndiko kuliko na waathirika wengi wa HIV kutokuweopo na usawa wa kijinsia, ukatilili wa kijinsia na kunyimwa haki kunawafanya wanawake wengi na wasichana kuwa hatika hatari kubwa ya kuambukizwa HIV.

Amesema hali hii inalitia mashaka makubwa bara la Afrika ambalo lina watoto zaidi ya milioni mbili wanaoishi na HIV na yatima zaidi ya milioni 15. Amesema mabadiliko katika sheria yatasaidia kudhibiti hali hiyo, George Njogopa na taarifa kamili

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Rais huyo amesema kuwepo kwa sheria kali kwa baadhi ya nchi kama zile zinazotoa adhabu kali kwa wale wanaobainika kusambaza virusi vya ugonjwa huo siyo mwarubani wa kukabilia hali ya maambukizi hayo.

Ametaka bunge liendelea kutumika kama chombo kinachoweza kupembua mambo na kutumia fursa kadhaa ikiwemo, maadili ya kiutu, mifumo ya maisha na hulka za kijamii ambazo zinaweza kutoa mchango mkubwa kuzua maambukizi hayo bila kutegemea sheria kali na ngumu zinazotumika kwa baadhi ya nchi.