Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya amani ya Darfur yaanza tena:UM

Mazungumzo ya amani ya Darfur yaanza tena:UM

Kundi la wapatanishi wakiwemo Umoja wa Mataifa , Muungano wa Afrika na Qatar wamewasili kwenye jimbo lililokubwa na mzozo la Darfur nchini Sudan wakati wa kuanza kwa mazungumzo yatayochukua siku kadha ya kuendeleza kupatikana kwa amani katika jimbo hilo.

Mpatanishi mkuu wa Umoja wa Mataifa na muungano wa afrika Djibrill Bassolé pamoja na waziri wa mashauri ya kigeni nchi Qatari Ahmed bin Abdullah Al-Mahmoud walianzisha mazungumzo hayo kwenye mji wa El Fasher ulio pia makao makuu ya kikosi cha pamoja cha UM na Muungano wa Afrika kulinda usalama katika jimbo la Darfur UNAMID hapo jana. George Njogopa na taarifa kamili

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Jopo la wapatanishi katika mzozo wa jimbo la Darfur nchini Sudan wamekuwa na mazungumzo na mwakilishi maalumu wa vikosi vya kimataifa UNMID Ibrahim Gambari kujadilia hatua zilizopigwa kwenye utanzuaji wa mzozo huo.

Wasuluhishi hao ambao kwenye mkutano huo uliwajumuisha pia wawakilishi kutoka makundi ya kijamii wamekuwa na kazi ya kusikiliza maoni toka pande mbalimbali kabla ya kuandaa ripoti maalumu iyatotoa mapendekezo kuhusiana na hali ya baadae ya eneo hilo.

Mapema mwezi septemba kamati hiyo ilitoa ripoti yake ya awali iliyozingatia namna ya kumaliza mapigano kwenye jimbo hilo la Darfur ambalo limeshuhudia umwagikaji mkubwa wa damu. Kiasi cha watu 300,000 wamepoteza maisha yao tangu kuzuka kwa mzozo huo na wengine milioni 2.7 wakilazimika kuyakimbia makazi yao.