Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Uganda azuru Somalia na kuahidi kuisaidia nchi hiyo

Rais wa Uganda azuru Somalia na kuahidi kuisaidia nchi hiyo

Chini ya masaa ishirini na manne baada ua bunge la Somali kupiga kura ya kutokuwa na imani na baraza la mawaziri lililoteuliwa na waziri mkuu Mohamed Abdullahi Mohamed, rais wa UgandaYoweri Museven alifanya ziara mjini Mogadishu ambapo alikutana na mwenzake rais wa Somali Sharif Sheikh Ahmed, Spika wa bunge la Somali Sharif Hassan Sheikh Adan pamoja na waziri mkuu Mohamed Abdullahi Mohamed.

Akiandamana na maafisa wa jeshi la Uganda rais Museveni aliwashukuru viongozi wa serikali ya Somali kwa kumaliza mzozo wa kisiasa uliubuka bungeni na kupelekea kupigwa kura ya imani dhidi ya baraza jipya la mawaziri. Pia aliwahakikishia kuwa serikali ya Uganda itaendelea kuwaunga mkono n kuwasaidia kwa kila njia.

Kwa upande wake raia Sharif wa Somali alimshukuru rais Museveni kwa ziara yake ambayo ni ya kwanza kwa kiongozi aliye madarakati kwa karibu miaka ishirini iliyopita Ambapo pia viongozi hao walizungumzia njia za kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi hizo mbili.