Hali ya hatari yatangazwa Guinea baada ya ghasia:OHCHR

19 Novemba 2010

Maafisa wa usalama wamewaua takriban watu wanne na kuwajeruhi zaidi ya wengine 300 kwenye mji mkuu wa Guinea Conakry kufuatia ghasia zinazohusishwa na kurudiwa kwa uchaguzi wa urais.

Afisi ya tume ya haki za binadamu OHCHR inasem kuwa imeshuhudia maafisa wa usalama wakiwapiga , kuwashika na kuwafyatulia risasi raia kwenye sehemu kadha za mji mkuu. Msemaji wa OHCHR Rupert Colville anasema kuwa baadhi ya ghasia hizo ni za kikabila.

(SAUTI YA RUPERT COLVILE TUTAISOMA HUKU)

Kiongozi wa upinzani Alpha Conde alishinda awamu ya pili ya uchaguzi wa urais uliondaliwa tarehe saba mwezi huu. Mapema juma hili Umoja wa Mataifa ulitoa wito kwa wananchi wa Guinea kukubali matokeo hayo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter