Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika Kusini inahitaji kupiga hatua kufanyia mabadiliko askari mamluki na kampuni za ulinzi :UM

Afrika Kusini inahitaji kupiga hatua kufanyia mabadiliko askari mamluki na kampuni za ulinzi :UM

Mwenyekiti wa kundi la Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya mamluki Alexander Nikitin anasema kuwa serikali ya Afrika Kusini inahitaji kufanya juhudi kufanya mabadiliko kwenye askari mamluki na kampuni za ulinzi zinazopeleka huduma zao nchi za ngambo.

Hii ni baada ya kundi hilo kufanya ziara yake nchini Afrika Kusini kwenye miji ya Cape Town na Pretoria. Kundi hilo limeshukuru serikali ya Afrika Kusini kwa mwaliko wake na pia kuwashukuru waliofanya mikutano nao zikiwemo idara za umma , polisi , wabunge , wasomi , waandishi wa habari na waakilishi wa sekta ya ulinzi. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)