Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutasalia Somalia fedha na vifaa vikipatikana:Jeshi la Burundi

Tutasalia Somalia fedha na vifaa vikipatikana:Jeshi la Burundi

Serikali ya Burundi imesema vikosi vyake vya kulinda amani vilivyojumuishwa kwenye vikosi vya muungano wa Afrika AMISOM nchini Somalia visalia endapo tuu msaada na mahitaji muhimu yakipatikana.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameyasema hayo kwenye mkutano wa kutathimini hali na msaada wa Somalia uliomalizika leo mjini Bujumbura Burundi na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa ambao umekiri kuwa vikosi vya AMISOM vinahitaji fedha na vifaa kutekeleza wajibu wake Somalia. Ramadhani Kibuga anachambua zaidi katika makala hii.