Skip to main content

Utapiamlo wasababisha vifo vingi vya watoto Yemen

Utapiamlo wasababisha vifo vingi vya watoto Yemen

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa idadi kubwa ya watoto wanaendelea kufa nchini Yemen kutokana na utapiamlo unaosababishwa na kuongezeka kwa mizozo na kuzorota kwa usalama.

Kulingana na utafiti mpya uliondeshwa na UNICEF unaonyesja kuwa asilimia 60 ya vifo vya watoto nchini Yemen vinasababishwa na utapiamlo. UNICEF linasema kuwa hali hiyo ni mbaya zaidi kwenye sehemu zilizoathirika na mozozo ambapo watoto weng ukosa chakula wakati shughuli za masomo nazo zikiathirika. Marixie Mercado ni kutoka UNICEF. (SAUTI YA MARIXIE MERCADO)