Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO na kampuni ya L'Oreal kuwatunuku wanawake wanasayansi

UNESCO na kampuni ya L'Oreal kuwatunuku wanawake wanasayansi

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya elimu, sayansi na utamadunI UNESCO limewatangaza wanawake 5 ambao wametoa mchango mkubwa kwenye masuala ya sayansi.

UNESCO kwa kushirikiana na kampuni moja ya vipodozi L'Oréal inatazamia kuwatunuku wanawake hao kama ishara ya kutambua mchango wao ambao umefaidia jamii.

Wanawake hao ambao wamekuwa wakiendesha utafiti wa mara kwa mara, wanatazamiwa kuondoka na kitita cha dola 100,000 kila moja, wakati wa sherehe za kuwatunuki zitakazofanyika makao makuu ya UNESCO Paris,Ufaransa hapo marchi 3, mwakani. Jumla ya wanasayansi 1,000 duniani kote walijitokeza kuwania nafasi hiyo.