Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano mapya yazuka Myanmar:UNHCR

Mapigano mapya yazuka Myanmar:UNHCR

Mapigano mapya yamezuka Mashariki mwa Myanmar kati ya majeshi ya serikali na waasi wa kikabila wa Karan kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Zaidi ya watu 18000 wamesambaratishwa na machafuko hayo yaliyowafanya kukimbia, kuvuka mpaka na kuingia Thailand. Mapigano hayo kwenye eneo la Myawaddy Mashariki mwa Myanmar yamearifiwa kuzuka muda mfupi baada ya uchaguzi wa Jumapili nchini humo.

Andrej Mahecic kutoka UNHCR anasema mashirika ya misaada ya kibinadamu yameanza kugawa msaada kwa wakimbizi wa ndani.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)

Nalo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema limesafirisha wakimbizi takriban 5000 wa Myanmar waliokuwa mpakani kwenye upande wa Thailanda hadi mahali pa usalama palipotengwa na serikali ya Thailand.