Ugaidi bado ni tishio kubwa Kusini Mashariki mwa Asia:UM

Ugaidi bado ni tishio kubwa Kusini Mashariki mwa Asia:UM

Ugaidi bado unatajwa kuwa tisho kubwa kusini mashariki mwa Asia hata baada ya mitandao ya kigaidi kupata pigo kufuatia ushirikiano uliopo wa kuzuia mashambulizi ya kigaidi.

Washirika kwenye warsha iliyondaliwa mjini Bali nchini Indonesia walisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa uangalifu na kwa jamii ya kimataifa kutoa usaidizi kwa nchi katika eneo hilo ili zipate kukabiliana na ugaidi.

Warsha hiyo ya Bali ni ya kwanza kati ya warsha tano zitakazoandaliwa zilizo na lengo la kuuunga mkono kutekelezwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na ugaidi lililopitishwa mwaka 2006.