Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kupeleka wataalamu wa mihadarati Kyrgystan

UM kupeleka wataalamu wa mihadarati Kyrgystan

Afisa wa Umoja wa Mataifa anashughulika na masuala ya madawa ya kulevya amesema leo kuwa atapeleka ujumbe wa watu nchini Kyrgyzstan kwa ajili ya kufanya tathmini juu ya hatua zipo zichukuliwe ili kuweza kukabiliana upitishwaji wa madawa ya kulevya toka Afghanistan na kuingizwa katika eneo la Asia na kati.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa juu ya madawa ya kulevya na vitendo haramu Yury Fedotov amesema kuwa hatua ya kupelekwa kwa wataalamu hao ni kuafiki ombi lililotelewa na Kyrgyzstan iliyotaka kupatiwa wataalamu hao.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa Afghanistan imeendelea kuwa kitovu cha utumiaji na usambazaji wa madawa ya kulevya aiana ya opium na hivyo kuendelea kutishia eneo nzima la ukanda huo. Hata hivyo ameeleza kuwa wataalamu hao mara watakapokamilisha ziara yao wanakusudia kuandaa mpango mkakati ambao utatumika kudhibiti kuenea kwa madawa hayo.