Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kutathimini visa zaidi ya 300 vya watu kutoweka

UM kutathimini visa zaidi ya 300 vya watu kutoweka

Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na kutoweka kwa hiyari ay kwa lazima WGEID kimeanza kutathimini zaidi ya matukio 300 ya watu kutoweka.

Kitengo hicho hivi karibuni kimewasilisha taarifa ya matukio yaliyokubalika awali na mawasiliano mengine yanayohusu nchi 40.

Katika kikao chake cha 92 kilichoanza leo hadi tarehe 12 Novemba mjini Geneva jopo la wataalamu binafsi wa kitengo hicho watabadilishana mawazo katika visa hivyo na kuvitathimini kwa kuwa na mikutano na wawakilishi wa serikali mbalimbali, mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa, familia za waliotoweka na wawakilishi wa jumuiya za kijamii.

Tangu kuanzishwa tarehe 29 Februari mwaka 1980 na tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kimeshashughulikia visa zaidi ya 50,000 vya watu kutoweka. Tarehe 5 Novemba mwaka huu kitengo hicho kitasherehekea miaka 30 tangu kuanzishwa.