Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shangai expo kusadia kutatua changamoto za dunia:Ban

Shangai expo kusadia kutatua changamoto za dunia:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyataja maonyesho ya kimataifa yaliyoandaliwa mjini Shanghai nchini China kuwa yenye umuhimu mkubwa katika kutatua changamoto za siku hizi zikiwemo za ukuaji wa haraka wa miji , mabadiliko ya hali ya hewa, na maendeleo.

Zaidi ya watu milioni 70 kutoka nchi mbali mbali walizuru maonyesho hayo ambayo ni kwanza kuandaliwa kwenye nchi inayoendelea yenye kauli mbiu "mji mwema maisha mema".Akiwa mjini Shanghai Ban ameitaja kauli mbiu hiyo kuwa iliyokuja wakati unaofaa akisema kuwa nusu ya watu walioko duniani wanaishi mijini na idadi hiyo itaendelea kuongezeka.

Ban amesema kuwa maonyesho hayo yaliwawezesha ,mamilioni ya watu kujifunza uwezekano wa kufanya miji yao kuwa iliyo na afya na salama na pia miji ambayo inawapa wenyeji wake hewa safi na maji na maisha mema.

Hata hivyo Ban ameongeza kuwa mabilioni ya watu bado wanaishi katika hali inayohatarisha maisha yao hususan wanaioishi sehemu za mabanda ambazo zimekosa mahitaji kama vile maji , makao mema na mazingira safi.