Skip to main content

Ban atoa wito wa kutaka kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa nchini Myanmar

Ban atoa wito wa kutaka kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa nchini Myanmar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa serikali ya Myanamar akiitaka iwachilie huru wafungwa wa kisiasa akisema kuwa bado kuna muda wa kuchukua hatua za kuleta uwiano wa kitaifa.

Akiongea mjini Hanoi nchini Vietnam anakohudhuria mkutano kati ya muungano wa nchi za kusini mwa Asia ASEAM na Umoja wa Mataifa, Ban amesema kuwa mashirika hayo mawili yamekubaliana kuwepo kwa mabadiliko ya kidemokrasia na uwiano wa kitaifa nchini Myanmar nchi ambayo inatarajia kuandaa uchaguzi mkuu tarehe saba Mwezi Novemba.

(SAUTI YA BAN)

Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaisadia Myanmar kulingana na uwezo wake ili iweze kusonga mbele kwa amani kwenda kwa awamu mpya ya kidemokrasia na maendeleo. Akitoa ripoti yake kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjumbe maalum kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Myanmar amesema kuwa haki ya kuzungumza na kukutana bado imebanwa na sheria za uchaguzi zilizotangazwa na tume ya uchaguzi.