Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Thailand yapata tuzo kuokoa maisha ya chui:CITES

Thailand yapata tuzo kuokoa maisha ya chui:CITES

Katibu mkuu wa mkataba wa biashara ya kimataifa kwa viumbe vilivyo hatarini Flora na Fauna CITES leo ametangaza kuwa amefanya uamuzi wa kuitunuku serikali ya Thailand kwa juhudi za kulinda viumbe hao.

Amesema tuzo ya vyeti itakwenda kwa kampuni ya umma ya uwanja wa ndege wa Thailand, vituo vya mbuga za wanyama za nchi hiyo, idara ya uhifadhi wa wanyamapori na misitu ya serikali ya Thailand katika uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi mjini Bankok.

Amesema vyeti hivyo vinatolewa kwa kutambua na kuthamini juhudi zao za kukamata na kunusuru maisha ya mtoto wa chui baada ya maafisa wawili wa uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi kubaini mtu aliyekuwa akitaka kumsafirisha kiharamu chui huyo aliyekuwa hai nje ya nchi Agosti 2010.

Chui huyo alikuwa mefungwa vizuri ndani ya mzigo na alibainika wakati kukagua mizigo kwa kutumia mashine maalumu. Tangazo hilo limetolewa wakati wa tukio maalumu la uhifadhi wa chui kwenye mkutano wa 10 wa kuhusu uhifadhi wa bayo-anuai unaofanyika mjini Nagoya Japan.