Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimo lazima kizingatie mabadiliko ya hali ya hewa:FAO

Kilimo lazima kizingatie mabadiliko ya hali ya hewa:FAO

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO imetoa wito kwa kilimo cha nchi zinazoendelea kwenda sambasmba na hali ya hewa ili kukabiliana na changamoto za ongezeko la idadi ya watu na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mabadiliko ya hali ya hewa yanatarajiwa kuathiri uzalishaji wa kilimo, usalama na uchumi wa nchi nyingi ambazo tayari zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula. Hata hivyo ripoti hiyo inasema uzalishaji wa kilimo duniani lazima ukuwe kwa asilimia 70 katika miongo mine ijayo ili kukidhi mahitaji ya chakula ya idadi ya watu inayoongezeka. George Njogopa na taarifa kamili

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

FAO imesema kuwa matatizo ya tabia nchi yataendelea kuiandama dunia ikiwemo kushuka kwa kiwango cha uzalishaji kwenye kilimo, pamoja na kukosekana kwa hali ya utengamano na kushuka kwa kipato. Imekadiria kwamba mahitajio ya dunia kwenye chakula ni makubwa hivyo yatalazimika yakuwe kwa kiwango cha asilimia 70 katika kipindi cha miaka minne ijayo ili kukidhi hitajio la ongezeko la watu duniani.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa FAO anayehusika na chakula Alexander Mueller, amesema kuwa pamoja na hitajio hilo la chakula, lakini ulimwengu lazima utambue kwamba unawajibika kuendeleza kilimo makini na salama kwa mazingira