Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya hali ya hewa lazima yapate suluhu:Figueres

Mabadiliko ya hali ya hewa lazima yapate suluhu:Figueres

Mjadala wa ngazi ya juu wa biolojia-anuai unaendelea mjini Nagoja Japan huku suala la mabadiliko ya hali ya hewa likipewa nafasi kubwa.

Mjadala huo unahudhuriwa na mawaziri wa mazingira na wawakilishi kutoka nchi takriban 100, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa mazingira. Viongozi hao wanajadili hatua zilizopigwa katika kutekeleza malengo ya uhifadhi wa bayo-anuai tangu kupitishwa mkataba mwaka 2002.

Pamoja na kuzingatia athari za kutoweka kwa bayo-anuai katika uchumi, biashara na maisha ya watu , suala la mabadiliko ya hali ya hewa na uhifadhi wa bayo-anuai limepewa uzito mkubwa. Katibu mkuu mtendaji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa UNFCCC Christina Figueres anasema serikali zimejifunza kwamba suala la mabadiliko ya hali ya hewa linahitaji muafaka na sio la lele mama.

(SAUTI YA CRISTINA FIGUERES)

Bi Figueres ameongeza kuwa anaelewa serikali zimebadili mtazamo tangu kufanyika kwa mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa mjini Copenhagen denmark mapema ambapo viongozi walidhani kungeweza kuwa na suluhisho la mara moja na tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa.