Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu Iraq:Pillay

Kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu Iraq:Pillay

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulia masuala ya haki za binadamu amesema kuwa nyaraka iliyofichua vita vya Iraq, imefumbua namna haki za binadamu zilivyokiukwa na kuleta udhalilishaji mkubwa kwa utu wa binadamu.

Kwa mujibu wa taarifa yake kuhusiana na kufichuliwa kwa nyaraka hizo, Bi Navi Pillay amesema kuwa hatua hiyo imekwenda kinyume na sheria za kimataifa zinazohusu haki za binadamu, hasa kuzingatia kuwa nyaraka hizo zinaonyesha namna wananchi wa Iraq walivyoteswa na kunyanyasawa na hata wale waliwekwa kuzuizini walipatiwa huduma mbaya kuliko.

Pillay amelalamikia kitendo cha vikosi vya Kimarekani kuwakabidhi watuhumiwa iliyokuwa ikiwashikilia kwa vikosi vya Iraq, licha ya kwamba ilikuwa ikifahamu kufanyika kwa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu kulikofanywa na vikosi vya Iraq.

Ametaka wale wote waliohusika kwa pande mbili vikosi vya marekani na Iraq wachunguzwe na kisha kufikishwa kwenye mkondo wa sheria.