Skip to main content

Nchi nyingi duniani bado zinaendeleza mateso:UM

Nchi nyingi duniani bado zinaendeleza mateso:UM

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mateso amesema kuwa nchi nyingi duniani bado zinaendeleza mateso.

Akiwasilisha ripoti yake ya mwisho juma hili kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Manfred Nowak amesema kuwa kati ya nchi tatu alizozuru mwaka huu zikiwemo Jamaica , Papua New Guinea na Ugiriki bado kuna visa vya mateso.

Bwana Nowak aliwaambia waandishi wa habari kuwa kati ya nchi 18 zilizomwalika kufanya utafiti kuhusu suala hilo ni nchi ya Denmark na Greenland ambazo hakuzipata kuendeleza mateso. Amesema kuwa nchi alizochunguza kutoka sehemu mbali mbali duniani na kutoka tamaduni na dini tofauti zinawakilisha theluthi kumi ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.