Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asia na Pacific hatarini kutokana na majanga asili:UM

Asia na Pacific hatarini kutokana na majanga asili:UM

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa nchi zilizo barani Asia na maeneo ya Pacific ziko kwenye hatari ya kukumbwa na majanga ya kawaida kuliko zingine zilizo maeneo mengine ya ulimwengu huku watu wanaoishi kwenye nchi hizo wakiwa na uwezekano mara nne zaidi ya kuathiriwa na majanga hayo kuliko wanaoishi barani Afrika na mara 25 kuliko watu wanaoishi barani Ulaya au Amerika.

Kulingana na ripoti ya tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya uchumi na jamii kuhusu majanga barani Asia na Pacific mwaka 2010 inasema kuwa majanga ya kawaida yamekuwa kizingiti kwa maendeleo kwenye maeneo hayo.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alisisitiza umuhimu wa kujiandaa kwa majanga wakati wa kuweka sera za maendeleo ya kitaifa. Ban amesema kuwa kuwa kutolewa onyo la mapema , hamasisho kwa umma na mipangilio bora mijini vyote vinaweza kupunguza athari zinazosababishwa na majanga hayo.