Bayo-anui ni muhimu sana katika maendeleo:UNEP

Bayo-anui ni muhimu sana katika maendeleo:UNEP

Mjadala wa ngazi za juu wa baolojia-anuai umeanza leo mjini Nagoya Japan. Mjadala huo unahudhuriwa na mawaziri wa mazingira kutoka takriban nchi 100, mashirika ya Umoja wa Mataifa kama lile la mazingira UNEP na Bank ya dunia.

Viongozi hao wa serikali na mashirika wanajadili hatua zilizopigwa katika malengo ya bayo-anuai yaliyowekwa na wadau wa mazingira mwaka 2002 walipopitisha mkataba. UNEP inasema taasisi za fedha duniani zimeanza kutambua ongezeko la athari za uwekezaji kutokana na kutoweka kwa bayo-anuai, katika miezi 12 iliyopita kupungua kwa bayo-anuai kumeathiri biashara kwa dola bilioni 10 hadi bilioni 50.

Mkurugenzi mkuu wa UNEp Achim Steiner amesema matatizo yanayojitokeza na ongezeko la athari vinadhihirisha mabadiliko yanayohitajika kwenye taasisi za fedha na makampuni yanayotegemea malia asili ambayo yameanza kubaini umuhimu wa bayoanuai katika uchumi.

Rais wa bank ya dunia Robert Zoellick anasema bayo-anuai ni muhimu sana katika uchumi.

(SAUTI ROBERT ZOELLICK)