Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aipongeza Thailand kwa kujihusisha na amani

Ban aipongeza Thailand kwa kujihusisha na amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza juhudi za serikali ya Thailand kujihusisha na mipango ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.

Ban ambaye amekuwa katika ziara ya siku mbili nchini humo amesema kitendo cha Thailand kutoa kikosi cha wanajeshi cha kwanza kabisa ambacho sio cha Afrika kwenda Darfur ni mfano wa kuigwa.

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari baada ya kukutana na viongozi wa serikali ya nchi hiyo akiwemo waziri mkuu Abhisit Vejjajiva Ban ameiomba serikali ya Thailand kuongeza maafisa wa polisi wanawake katika operesheni za kulinda amani.

(SAUTI BAN KI-MOON)

Ban ambaye anaendelea na ziara ya Asia na Pacific leo ameondoka nchini Thailand kwenda Cambodia na kisha Uchina kabla ya kurejea tena Bankok Thailand kwa ajili ya mkutano wa nchi za Asia-Pacific kama maandalizi ya mkutano wa mwezi ujao wa G20.