Ban atoa msukumo wa kuvisaidia vikosi vya AU
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza haja ya kutoa msaada kwa vikosi vya kulinda amani vya Muungano wa afrika kama ule unaotolewa kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa.
Ban ametoa msisitizo huo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo lililpokuwa likijadili masuala ya amani na usalama barani Afrika. Ban amesema muungano wa Afrika au AU unaendelea kukabiliwa na matatizo ya kupata fedha na vifaa muhimu ili kusaidia shughuli zake za kulinda amani katika maeneo kama Darfur na Somalia.
Ameongeza kuwa tunahitaji kupata suluhisho ambalo litawezesha kupatikana kwa msaada unaoaminika na kutosheleza mahitaji ya vikosi vya muungano wa afrika wakati inapofanya operesheni za kulinda amani zilizoidhinishwa na baraza la usalama chini ya kifungu namba saba kwenye mkataba wa amani kama ilivyo kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa.