Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washitushwa na ujenzi mpya wa makazi Ukingo wa Magharibi

UM washitushwa na ujenzi mpya wa makazi Ukingo wa Magharibi

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ametoa tahadhari kuhusu ripoti za ujenzi wa makazi mapya ya Israel kweenye ardhi ya Wapalestina akionga kuwa ujenzi huio mpya utaleta madhara zaidi baada ya kukwama kwa mazunguzo ya moja kwa moja katika ya Palestina na Israel.

Robert Serry mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye mpango wa amani wa Mashariki ya Kati ujenzi hu ambao ni kinyume na sheria za kimataifa pia unakiuka wito wa jamii ya kimataifa wa kutaka pande hizo kubuni mazingira mema kwa mazungumzo.

Muda Israel iliweka wa kusitisha ujenzi wa mmakaazi hayo ulifikia kikomo mwezi uliopita hata baada ya Umoja wa Mataifa , Jumuiya ya Ulaya na Urusi kuishawishi kutoendelea na ujenzi huo.Naye rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema kuwa hataendelea tena na mazungumzo hayo hadi pale Israel itakapositisha ujenzi huo.