Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taasisi mpya kuchunguza masuala ya uhamiaji kuzinduliwa

Taasisi mpya kuchunguza masuala ya uhamiaji kuzinduliwa

Taasisi mpya ambayo itahusika na utafiti wa uhamiaji katika maeneo ya Afrika , Caribbean na Pacific itazinduliwa rasmi juma lijalo kwenye mji mkuu wa Belgiam Brussels.

Mpango huo uanofahamika kama ACP unazileta pamoja nchi 79 kutoa Afrika ,Caribbean na Pacific na utasimamiwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na washirika wengine 15 na kupata ufadhili wa Euro bilioni 8 kutoka kwa jumuiya ya ulaya. Uswisi na IOM, George Njogopa na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Taasisi hiyo inatazamiwa kutoa mchango mkubwa kukabiliana na wimbi la ongezeko la watu wanahama toka nchi zao na kuelekea nchi za Ulaya na kwingineko duniani. Itafanya utafiti kubaini kiini cha tatizo hilo na pia kutoa ushauri wa kisera kwa ajili ya maendeleo.

Uzinduzi huo unatazamiwa kuhudhuriwa na wageni waalikwa 200 kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, ikiwemo pia wanadiplomasia, taasisi za kiserikali na zile za kirai pamoja na taasisi zinazohusika na masuala ya uhamiaji.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaohama nchi zao na kwenda kuomba hifadhi katika nchi za Ulaya.Mwaka jana pekee watu 11,000 waliomba hifadhi ya ukazi katika nchi zilizopo kwenye jumuiya ya Umoja wa Ulaya, ikiwa ni ongezeko la asilimia 13, ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2008.