Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa UM kwenda Sahara Magharibi wawasili Algeria

Ujumbe wa UM kwenda Sahara Magharibi wawasili Algeria

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Sahara magharibi umefanya mazungumzo nchini Algeria kama moja ya juhudi za kutatua mzozo wa muda mrefu ambao umeshuhudiwa tangu mwaka 1976 wakati kulipozuka mapigano kati ya Morocco na Frente Polisaria ulipoisha utawala wa kikoloni wa Hispania.

Baada ya kukutana na rais wa Senegal Abdelaziz Bouteflika mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Christopher Ross aliwaambia waandishi wa habari kuwa ziara hiyo ina lengo la kuondoa vizuizi kwa mazunguzo kati ya Morocco na Frente Polisario.

Ross amesema kuwa kunahitajika kufanyika kwa mazunguzo bila ya vikwazo ili kupatikana kwa suluhu la kudumu kwa watu wa Sahara Kusini. Morocco imewasilisha mpango wa kutaka kulitawala eneo la Frente Polisario wakati ambapo eneo hilo likishikilia kuwa hali yake itaamuliwa kupitia kwa kura ya maoni ukiwemo uhuru kama uamuzi wa mwisho.