Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesi ya Jean Pierre Bemba itaendelea Hague:ICC

Kesi ya Jean Pierre Bemba itaendelea Hague:ICC

Kitengo cha rufaa cha mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC leo kimetoa uamuzi kuhusu hatama ya kesi ya aliyekuwa makamu wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean Pierre Bemba.

Kitengo hicho kimesema sasa kesi ya Bemba ambayio imeahirishwa mara mbili itaendelea. Bemba anakabiliwa na mashitaka mawili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na mashitaka matatu ya uhalifu wa vita anaodaiwa kutekeleza kwa kuongoza kundi la wanamgambo kwenye nchi jirani ya Afrika ya Kati kati ya mwaka 2002 na 2003.

Awali mawaikili wake walitoa wito wa kesi dhidi ya Bemba kufutwa lakini majaji wa kitengo cha rufaa hawakukubaliana kuhusu ombi hilo. Bemba alikamatwa 2008 nchini Ubeligiji na kusafirishwa hadi The Hague.