Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imeanza kuwarejesha wakimbizi wa Mauritania

UNHCR imeanza kuwarejesha wakimbizi wa Mauritania

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR jana Jumatatu limeanza zoezi la kuwarejesha wakimbizi wa Mauritania walioko Sengal baada ya mapumziko ya miezi kumi.

UNHCR imesema imesafirisha kundi la kwanza la abiria 121 hadi mjini Rosso Kusini mwa Mauritania baada ya kuvuka mto Senegal ambo ni mpaka baina ya nchi hizo mbili. Jayson Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

UNHCR inasema ilirejelea shughuli hiyo kufuatia mazungzo na serikali ya Mauritania na baada ya kumalika kwa msimu wa mvua. Inasema kuwa inapanga kuwasafirisha nyumbani wakimbizi 2500 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Wakimbizi kutoka Mauritania wamekuwa wakiishi nchini Senegal kwa zaidi ya miongo miwili .

Kuanzia juma hili serikali ya Mauritania imechukua jukumu la kuwasafirisha raia wake wanaorejea nyumbani kwenda maeneo ya mwisho na kuwapa makazi ya muda na pia bidhaa za ujenzi sawia na kuwapa vyakula.

Wakimbizi hao ni kati ya melfu ya wengine waliokimbia makwao kulipozuka mzozo wa mpaka kati ya Mauritania na Seneagal mwaka 1989. Bado wakimbizi 21,300 wa Mauritania wanaishi nchini Senegal wakati wengine 10,500 wakiishi nchini Mali.