UM waonya kuhusu kuongezeka kwa uhalifu uliopangwa duniani
Afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kupambana na uhalifu ametaka kutekelezwa kwa makubaliono yaliyoafikiwa ili kupambana na hali hiyo.
Yury Fedotov mkurugenzi wa idara ya UM inayohusika na madawa na uhalifu UNODC amesema kuwa uhalifu uliovuka mipaka umeongezeka kote duniani. Kwa sasa nchi kadha zimekusanyika mjini Vienna kwenye mkutano wa juma moja kutathimini hatua zilizopigwa muongo mmoja baada ya makubaliono ya kupambana na uhalifu uliopangwa yalipoafikiwa kwenye mji wa Palermo nchini Italia. Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo bwana Fedotov amesema kuwa hata kama makubaliono yana nguvu hayatumiki kwa njia inayofaa. Amesema kuwa hamasisho zaidi inahitajika ili kusaidia nchi kutumia ipasavyo makubaliono hayo.