Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna umuhimu wa ajira katika kumaliza umasikini:UM

Kuna umuhimu wa ajira katika kumaliza umasikini:UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa ajira ni muhimu katika kujenga jamii zinazoishi kwa amani.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kumaliza umasikini Ban amesema kuwa zaidi ya nusu ya watu wanaofanya kazi duniani ambao ni karibu watu bilioni 1.5 wanafanya kazi katika mazingira mabaya na kulipwa mishahara midogo. Zaidi ya watu milioni 60 kote duniani walilazimishwa kuingia kwenye umasikini na hali mbaya ya uchumi iliyoikumba dunia na ukosefu wa ajira kupanda wa thuluthi moja tangu mwa 2007. Ban amesema kuwa kuziba pengo lililopo kati ya umaskini na ajira nzuri kunahitaji kutumika kwa sera zinazo changia kuwepo kwa ajira , mazingira mazuri ya kufanyia kazi , usalama wa kazi na upatikanaji kwa urahisi kwa elimu, huduma za afya na mafunzo ya kikazi. Ban ametoa wito kwa vijana kutengewa nafasi za kazi akisema kuwa vijana hukabiliwa na tatizo la ukosefu wa jira kuliko watu wazima.