Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama Mashariki mwa DR Congo ni changamoto :UM

Usalama Mashariki mwa DR Congo ni changamoto :UM

Ukubwa wa eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unasababisha changamoto kubwa katika kulinda usalama wa raia .

Hayo yamesemwa na mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO bwana Roger Meece. Akitoa taarifa kwenye baraza la usalama mjini New York hii leo Meece amesema hivi sasa kuna zaidi ya vituo 90 vya MONUSCO katika maeneo yanayotajwa kama ni ya hatari.

Ameongeza kuwa licha ya vituo hivyo bado ni vigumu kuwalinda raia wote kutokana na ukubwa wa eneo, kwani makundi yenye silaha yanaendesha shughuli zake katika wigo mpana sio tuu katika vijiji na miji na mara nyingi yanajichanganya na raia. Katika eneo hilo ambalo ni kubwa kuliko Afghanistan amesema bwana Meece si rahisi kwa MONUSCO kuhakikisha ulinzi kamili kwa raia.