Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuchomwa kwa msikiti Mashariki ya Kati kwa ushangaza UM

Kuchomwa kwa msikiti Mashariki ya Kati kwa ushangaza UM

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa katika eneo la mashariki ya kati Robert Serry amelaani vikali kisa cha kuchomwa kwa msikiti katika eneo la ukingo wa magharaibi wa mto Jordan.

Kisa hicho kinakisiwa kutekelezwa na walowezi wa kiyahudi wanaopinga mpango wa amani kati ya Israel na Palestina ambao pia wanaripotiwa kufuru kuta za msikiti huo. Msemaji wa UM Martin Nesirky amesema kuwa sio tu suala la kushangaza bali kamwe kitendo cha kufuru kuta za msikiti hakitakubalika na kutoa wito kwa wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria .

Wakati huo nayo ofisi ya bwana Serry inaitaka serikali ya israrael kuhakikisha kuwa wale waliokufuru kuta za msikiti huo wamefikishwa mbele ya sheria.