Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya waalimu

Leo ni siku ya kimataifa ya waalimu

Leo ni siku ya waalimu duniani kauli mbiu ikiwa, maendeleo huanza na waalimu. Mwaka huu maadhimisho ya siku hii ni ya kuenzi mchango mkubwa wa waalimu katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kiakili.

Waalimu kutoka Haiti, Israel, Mali, Lesotho, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Lao na Ufaransa watabadilishana uzoefu wa kukabiliana na mtatizo kwenye mjadala maalumu ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO mjini Paris.

Pia mjini Paris kutatolewa takwimu za tatizo la upungufu wa walimu kimataifa na maonesho ya picha za waalimu wanaofanyan kazi katika mazingira magumu. George Haddad ni mkurugenzi wa kitengo cha elimu ya juu UNESCO.

(SAUTI YA GEORGE HADDAD)

Nao mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova, mkuu wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Helen Clark, mkurugenzi wa UNICEF Anthon Lake na mkurugenzi mkuu wa ILO Juan Somavia wametoa taarifa ya pamoja na kusema mishahara midogo, hadhi ndogo ya kazi hiyo, na mazingira mabaya ya kazi yayokiuka haki za waalimu yamewafanya vijana kutotaka kuingia katika fani hiyo, na wametaka matatizo hayo kushughulikiwa hasa sasa ambako dunia inahitaji waalimu wapya milioni 10.3 ili kuweza kufikia lengo la maendeleo la elimu ifikappo 2015.