Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu waelimishwe kuhusu usafirishaji haramu wa watu:IOM

Watu waelimishwe kuhusu usafirishaji haramu wa watu:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linaadhimisha mwaka wa tano wa wiki ya kuelimisha kuhusu usafirishaji haramu wa watu nchini Afrika ya Kusini.

Nchini Afrika ya Kusini wiki hii imeandaliwa na kitengo cha taifa cha sheria, idara ya mambo ya ndani, idarra ya elimu, wadau wengine wa serikali na jumuiya za kijamii. IOM ambayo inasaidia inasema lengo kubwa ni kuwakumbusha watu kuwa usafirishaji haramu ni kosa la jinai na ni suala linalohitaji ushirikiano kulidhibiti. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Afrika Kusin inajiandaa kuadhimisha wiki ya kukabiliana na vitendo vya usafirishaji binadamu na tayari Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM,limesema litaunga mkono maadhimisho hayo ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaelimisha zaidi wananchi. Maadhimidho hayo ambayo yanatazamiwa kufanyika juma hili, yana shabaha ya kuelezea athari na ubaya wa biashara ya kusafirisha binadamu.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ambayo ni ya tano kufanyika inasema kuwa " Usafirishaji wa binadamu upo kweli" Katika kutia msukumo kwenye maadhimosho hayo shirika hili la kimataifa la uhamiaji, limeazimia kushirikiana na taasisi kadhaa za kiserikali ikiwemo pia Wizara ya mambo ya ndani, idara ya mashtaka ya taifa pamoja na mashirika mengine ya kirai.

Hadi sasa tayari shamra shamra za maandalizi ya maadhimisho hayo zimeanza kupamba moto, na katika mitaa mbalimbali kumeanza kusambazwa mabango yenye ujumbe unaokemea biashara hiyo ya usafirishaji binadamu.