UM wasaidia kukabiliana na polio na minyoo Afghanistan

UM wasaidia kukabiliana na polio na minyoo Afghanistan

Takriban watoto milioni nane nchini Afghanistan wanatarajiwa kupata chanjo dhidi ya maradhi ya polio juma hili kama moja ya harakati zinazoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambayo pia itashulikia tatizo la minyoo miongozo mwa watoto wachanga nchini humo.

Makundi 22,000 ya kutoa chanjo yatashiriki kwenye kampeni hiyo ya siku tatu itakayoendeshwa kote nchini Afghanistan na kulenga zaidi vituo vya basi , misikiti , masoko na pia kuzuru nyumba hadi nyumba.

Shirika la afya dunianio WHO na lile la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, mashirika yanayoshirikiana na wiza ya afya nchini Afghanistan kuendesha kampeni hiyo yanasema kuwa kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kunahitajika kuhakikisha kuwa idadi kubwa zaidi ya watoto wamepata huduma hiyo.

 Afghanistan ni moja kati ya nchi sita zingine zikiwemo Pakistan , India na Nigeria ambazo zinaripoti visa vingi vya ugonjwa wa polio huku mataifa mengine yakiwa tayari yameungamiza ugonjwa huo. Mwakilishi wa WHO nchini Afghanistan Peter Graaff amesema kuwa kutolewa kwa pamoja kwa chanjo ya polio na pia dawa ya minyoo ni mradi mzuri kwa sekta ya afya ya nchini Afghanistan